Dialogue - Swahili

Hide

Vocabulary

Hide
kugombea contest
kale vintage, ancient
mshabiki enthusiast
pikipiki motorcycle
muktadha wa kimataifa global context

Lesson Notes

Hide

Cultural Insights

Jambo la Kufurahisha Kuhusu Tamasha la Concours D' Elegance




Mtalii mmoja wa Marekani alijiuliza kwa nini Kenya husisitiza kuhifadhi tamasha la Elegance D Concours. Kwa upande wake,  aliamini kwamba baadhi ya magari ya kale kamwe hayawezi endeshwa katika barabara mbovu za Kenya. Naam, alikuwa sahihi; mengi ya barabara ya Kenya yako katika hali mbaya. Hata hivyo alitishwa kuona idadi kubwa ya watazamaji ambao walifika kwanye tamasha hilo. Wakenya hupenda magari. Kama nchi hii inaweza kuwa na uwezo wa kiufundi na mtaji mkubwa unaohitajika kuanzisha viwanda vya kuunda magari; basi magari yenye utaalamu mkubwa yangekuwa yakiagizwa kutoka Kenya. Isitoshe, tulikuwa na gari letu la kwanza 'Gari la Kenya' mwaka wa 1986 lakini kwa bahati mbaya iliharibika baada ya robo saa ikiwa imefikisha mwendo wa juu zaidi wa kilomita 21 kwa saa.

 

Fun Fact About Concours D'Elegance


 

An American tourist wondered why Kenya insisted on preserving the Concours D' Elegance festival. She reasoned that some of the antique cars could never be driven on the poor roads of Kenya. Well, she was right—most of the Kenyan roads are in a poor state. She was shocked, however, to see the number of spectators who turned up to grace the occasion. Kenyans love cars. If only the country had the technical capabilities and the huge capital required to start its own car manufacturing factory, then the most technically developed cars would be imported from Kenya. We even had our first 'All Kenyan' car in 1986, but unfortunately, it broke down after exactly a quarter of an hour at a maximum speed of twenty-one kilometers per hour.

Lesson Transcript

Hide
Tamasha la Concours D’ Elegance.
Tamasha la Concours D’ Elegance linahusu mashindano ya uzuri wa magari kukiwamo maonyesho ya magari ya kifahari na pikipiki. Pia mna muziki na burudani isiyo na kikomo kwa watoto. Maonyesho haya hufanyika kila mwaka, mwezi wa Septemba katika uwanja wa ‘Race Course’ jijini Nairobi. Tamasha hii inayondaliwa na wanaomiliki klabu ya Alfa Romeo ilianza California mwaka wa 1910 na kisha nchini kenya baada ya miaka ishirini. Ni tamasha la kifahari zaidi na la aina yake ulimwenguni. Huonyesha uzuri na upekee iliyo katika magari ya zamani na pia iliyo kwenye bidhaa mengine ya magari ya kisasa. Wakati unaposalia, maonyesha haya yamevutia washiriki kutoka Australia, Uingereza, Ujerumani, Mauritius, Zimbabwe likiwa Afrika Kusini, Tanzania na Uganda. Tamasha hili linalojulika hasa kwa mtindo na historia unapenyeza modeli ya magari yaliyoundwa yapata miaka ya 1920. Ni katika tamasha hii pekee tunapoweza kuona magari ambayo huonyeshwa kwenya sinema pekee na ambazo hazitaweza kupatikana kwenye barabara za Kenya. Wanaomiliki baadhi ya magari haya na pikipiki hufurahia kuendesha magari yao mbele ya umati wa watazamaji waliofurika uwanjani. Gari la kifahari na pikipiki hunandaliwa kwenye uwanja wa mashindano kabla ya tamasha hili la magari; hivyo basi, kuwapa fursa nzuri watu wanaotaka kuuza magari yao kwa wanoataka kununua. Tukio hili huipa Taifa la Kenya jukwaa ya kuonyesha muktadha wa kimataifa kuwa kando na kuwa na mwamba mzuri na mambuga ya wanyama pori, una uwezo wa kuandaa matukio ya msimamo wa kimataifa. Tukio hili kubwa na ambalo huchukua siku moja huisha kwa kuwatangaza washindi kwenye vikundi mbalimbali. Kuna mshindi wa jumla na washindi katika viwango vingine kulingana na miundo na wakati wa kutengenezwa. Tathmini huanza kwa kuangalia upande wa chini, ikifuatwa na jinsi nje ilivyomaliziwa, kisha upande wa ndani na hatimaye mitambo.