Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

AVRIL
Judith Nyambura Mwangi ama Avril alizaliwa tarehe 30 mwezi wa Aprili mwaka wa 1986 mjini Nakuru, nchini Kenya.
Alifanya masomo ya sekondari nchini Kenya na kisha kuendelea na kidato cha tano na sita nchini Uganda.
Sasa ana shahada katika somo la kubuni bidhaa kutoka chuo kikuu cha Nairobi.
Amesaini na kampuni ya kurekodi inayo julikana kama Ogopa Deejays na ameweza kufanya kazi na wasanii wanao tambulika humu nchini Kenya na Afrika Mashariki.
Maisha ya Avril kama mwimbaji ulianza alipokua msichana mdogo.
Baadaye aliweza kuwa spika wa umma ambapo aliweza kuwa mchanaji katika sherehe za shule na akaendelea na mtindo huu hadi vidato vikuu shuleni.
Wakati huu alipokuwa shuleni, kiwanda cha muziki nchini Kenya kilikuwa changa.
Lakini kizazi cha kwanza cha wasanii wa Pop kutoka Ogopa Deejays (ambapo yuko hata sasa) walipokuchukua hatua mpya, Avril alihisi ubora wao na maramoja kujiunga nao.
Wakati huo ndipo aligundua kuwa alifaa kuwa mmoja wao.
Sauti yake ya kubuni huunda hisia kubwa ambazo zinaweza kuhusishwa kwa urahisi na vijana na pia wazee duniani kote kwa ajili ya uwezo wake wa kuunganisha miundo kadhaa ya muziki.
Hata hivyo, mwimbaji huyu aliuunda habari wakati picha zilizoonyesha uchi wake ziliweza kubandikwa na kutandazwa katika mtandao wa intaneti.
Inaaminika kuwa alizibandika picha hizi ili apate umaarufu kwa vile hakuwa nao kama alivyonao leo.
Aliyakanusha madai haya akidai kuwa hawezi kulifanya jambo kama hilo na kwamba picha hizo zilikuwa zimefanyiwa ukarabati na jamaa waliokuwa wanamwonea kijicho kwa kufaulu kwake.
Wakati huu alikuwa anamwona kisiri mchezaji santuri mmoja aliyekuwa tayari na uhusiano na mchumba wake.
Haya tuyaweke kando, aliuandika wimbo spesheli baaada ya vita vya uchaguzi nchini Kenya, ikiwa na lengo ya kuwaunganisha wakenya.
Hamu yake ni kua Kenya itaweza kukumbatia tofauti zake katika nyanja za ukabila na kufanya kazi kwa umoja.

Comments

Hide