Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mombasa
Mji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya ni Mombasa, ambao pia ni mojawapo ya kivutio maarufu cha utalii kote Afrika. Mji huu uko kulia mwa bahari ya Hindi, hivyo basi ni nyumbani mwa baadhi ya fukwe nzuri duniani na pia Bandari muhimu katika Afrika. Takriban watu milioni moja huishi ndani ya mji huu ambao umejitenga na hori mbili kutoka bara Afrika. Daraja ya Nyali unaunganisha kisiwa cha Mombasa na bara, ilhali daraja ya Makupa inaiunganisha kwa magharibi. Wasafiri wanaweza pia kuwasili katika kisiwa kwa kutumia Feri ya Likoni kusini mwa mji huu.Uchumi wa Mombasa unategemea nguzo mbili kuu: utalii na biashara. Kiingilio cha bandari ya Mombasa kina kina kirefu kwa sababu mamilioni ya miaka iliyopita kilimezwa na bahari wakati ngazi za bahari zilipopanda. Kiingilio hiki hasa hufanya biashara kuwa rahisi. Viwanda vingine vyenye ukubwa ambazo huchangia kwa uchumi wa mji huu ni kiwanda cha kusafisha mafuta na kile cha kutengeneza saruji cha Bamburi.Watalii wengi mjini Mombasa hasa huchukua muda mchache katikati ya mji. Badala yake wao hupatikana ukingoni mwa bahari ulio mwisho wa mji huu. Baadhi ya watalii hutembelea Mji Mzee au Ngome ya Yesu kama wana hamu ya kutazama maeneo haya wakiwa ndani ya mji. Ufukwe wa kaskazini wa mji umepambwa na burudani tosha, mengi ya maeneo haya huwa yamefunguliwa masaa ishirini na manne.

Comments

Hide