Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Siku ya mashujaa
Kwa kizazi kipya, siku kuu ya Kenyatta itabaki likizo ya umma ya kihistoria. Katiba mpya ilibadilisha jina la likizo hili na kulibandika sikukuu ya Mashujaa. Kwa miaka arobaini na moja iliyopita, siku hii imekuwa ikiadhimisha siku rais wa kwanza alitoka gerezani baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka saba. Pia inakumbuka watu wengine saba waliodaiwa kuwa viongozi wa mstari wa mbele wa dini iliyopigwa marufuku. Wasomi wengi wamesema kuwa tukio hili halikustahili kuwa likizo ya kitaifa. Watu hawa walikuwa wamekana kuhusika kwao katika jeshi la uasi ambalo lilisababisha vita vya ugaidi vilivyo mshinda mzungu. Baada ya uhuru kutangazwa, wasomi katika jamii walichukua kwa haraka viti vya juu serikalini na kutangaza kuanzishwa kwa likizo hii katika taifa nzima. Kwa maoni yangu, siku hii inapaswa iwe jumuisho la heshima kwa wanaume na wanawake wote, watoto na wazee ambao wamechangia kuzaliwa kwa taifa hii. Basi ilikuwa wazo kipaji kuibadlilisha siku hiyo kuwa siku ya mashujaa ya waliopigania uhuru na pia kuzingatia Wakenya wa kisasa ambao wameendelea kufanya nchi ing’ae kimataifa.Kila Oktoba 20, Wakenya hukaa chini na kutafakari kuhusu wanaume na wanawake jasiri walio changia kuwasaidia wakenya kujivunia utamaduni, uhuru, urithi na amani yao. Orodha ya mashujaa haina mwisho, hii ina maana kwamba Wakenya zaidi watakuwa wakiongezeka masiku yakizidi. Ingawa hakuna vigezo vya uteuzi wa mashujaa wa kweli, ni wazi kwamba Wakenya wengi wanathibitishia ulimwengu kwamba wao pia wanauwezo wa kujenga historia.

Comments

Hide