Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Mlima wa Longonot.
Kama unazuru nchi ya Kenya kwa mara ya kwanza, Mlima longonot ni mojawapo ya maeneo ambayo lazima uyazuru.Mlima huu uko karibu na mji wa Naivasha yapata kilometa sitini kutoka jiji la Nairobi.Mlima huu ni wa aina ya volcano lakini kwa muda mrefu haujalipuka na inasemekana mara ya mwisho kulipuka ulikuwa katika karne ya themanini.Mlima wa Longonot uko katika bonde la ufa na kimo chake ni mita 2776 juu ya bahari na ni kati ya vivutio vikuu vya watalii nchini Kenya. Kaldera iliyo juu ya mlima itakuvuta kutoka kwa barabara unapoelekea Naivasha kutoka Nairobi. Mlima Longonot ni mojawapo ya milima ambayo wakenya wanapenda kukwea. Itachukua takribani masaa mawili kupanda hadi kilele cha mlima kutoka kiingilio . Unapokwea huu mlima,kuna sehemu telezi ambazo utapitia na kwa hivyo inafaa uwe mzima kiaafya unapoenda kukwea.Sehemu maridadi utakazooona unapofikia kilele cha mlima zitafanya usahau uchungu wote uliopitia ukiukwea huu mlima. Zaidi ya hayo, mlima huu wote ni mbuga la wanyama linalomilikiwa na shirika la wanyama pori la Kenya. Kama wewe ni mpenzi wa wanyama, basi mlima longonot ni mahali bora pa kuenda likizo .Mbuga hili lina wanyama kama vile nyati, swala chui, na tembo kati ya wengine ambao wanaishi katika msitu mkubwa unaofunika mlima kutoka chini.Mlima huu pia hutoa nafasi nzuri kwa wanaopenda kupiga kambi. Ndani ya lima huu hakuna makaazi lakini unaweza pata mahoteli ya kifahari katika mji wa Naivasha ambao uko kilometa ishirini tu kutoka mlima huu.

Comments

Hide