Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

‘Maralal camel derby’
Tamasha za ‘Maralal camel derby’ zilianza kama mojawapo ya njia ya kuwapatanisha jamii katika Wilaya ya Samburu ambao wamekuwa wakipigana kwa miaka. Kadri muda unavyoenda shughuli hii imegeuka na kuwa kivutio kikubwa cha watalii, huku ikivutia washiriki na watazamaji duniani kote. Shughuli hii ambayo kwa kawaida huchukua muda wa siku tatu hufanyika kati ya agosti ishirini na nne na ishirini na sita kila mwaka katika kambi ya ngamia ya yale kaunti ya Samburu. Sherehe hii huhusisha shughuli mbalimbali zikiwemo mbio za ngamia kwa wanaoshiriki kwa mara ya kwanza yaani ‘amateurs’ na waliohitimu.Pia kuna mbio za ‘triathlon’ za kilomita kumi na pia kilomita tano kwa vilema.Tamasha hizi pia huhusisha mashindano ya mbio za baiskeli na pia nyimbo na densi za kitamanduni zikiwemo sherehe za kufunga doa. Huwa ni wakati mwema wa watu kushiriki katika tamaduni mbalimbali na kujivinjari. Wageni huanza kuwasili kutoka tarehe ishirini na moja. Hapa wanapata nafasi nzuri ya kutembelea maeneo kama “world end view” na “house of God”. Baada ya hapo wao hujisajilisha shughuli mbalimbali ambazo watakuwa wakishiriki . Kabla ya mashindano kuanza, wageni hupata nafasi ya kupewa masharti fulani watakayozingatia haswa wanaoshiriki kwa mara ya kwanza. Tamasha rasmi huanza siku ya Agosti 24 kwa mbio za ngamia kwa wanaojifunza. Mbio hizi huandamana na mashindano ya kuendesha baiskeli. Wageni hutumbuizwa kwa nyimbo na densi za kitamaduni wanapopata maankuli ya mchana.Baadaye mbio za walemavu pamoja na zile za ‘triathlon’ hufuata. Masaa ya usiku huwa ni wakati wa watu wote kukusanyika katika tamasha ya kusherehekea utamaduni wa wasamburu yaani “samburu night”. Siku ya tatu, ambayo ni siku ya mwisho ya tamasha, hubeba shughuli kadhaa zikiwemo mbio za masafa kwa vigogo na pia mbio za kuendesha baiskeli.Tamasha hizi hufika kilele kwa wageni kukusanyika na kutuzwa kwa waliong’ara katika nyanja mbalimbali.

Comments

Hide