Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

KUOKOLEWA KWA HELIKOPTA
Kitabu hiki kimeandikwa na K W Wamitila aliyezaliwa tarehe 13 Juni mwaka wa 1965.
Yeye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi.
Hii ni hadithi inayohusu kituko kizuri ambacho baadae kilienda mrama.
Katika kitabu hiki, Zeke, kijana wa umri wa miaka kumi amshawishi Kate, binamu yake aliyekuja kumtembelea, ya kuwa andamane naye hadi kisiwa kilichokuwa hapo karibu.
Wawili hawa waliondoka na kwenda kwa kile kisiwa bila kumfahamisha yeyote.
Dalili ya mvua ilikuwa wazi hapo tu walipowasili ziwani.
Zeke anaenda mbele na kumkaribia mvuvi mmoja anayemwomba awapeleke kisiwani bila malipo.
Kwa mara ya kwanza, mvuvi anasita kuwapeleka kwa vile anahisi kuwa kuendesha mashua katika hali ile mbaya ya anga ingekuwa ni hatari lakini anabadili mawazo yake Zeke alipozidi kusisitiza.
Mvuvi anawapeleka Zeke na Kate kwenye kisiwa na kurudi kuvuvi kwa haraka baada ya kuwafikisha pale kisiwani.
Peke yao, vijana hawa wawili wanaanza kuvumbua kisiwa hiki ambapo wanafanikiwa kupata pango lililo kuwa ndani ya mbuyu uliofaraghiwa.
Waliamua kuingia ndani zaidi ya ile pango ambamo walibebeka na mazuri yaliyokuwa ndani.
Kulikuwemo maandishi ya kigeni, alama za kusisimua kwenye kuta na mawe meusi zilizofanya akili za vijana hawa kuduwaa na kubebeka zaidi.
Mvua ulianza kunyesha kwa uzito na mvuvi akaondoka kwa haraka na kusahau kuwachukua vijana hawa.
Alikumbuka kuhusu vijana hawa mara tu alipofika ukingoni.
Kurudi katika kile kisiwa ili kuwaokoa Zeke na Kate ilikuwa haiwezekani kwa vile mvua ulivyokuwa ukinyesha kwa wingi, ndivyo hali ya hatari ilivyoendelea kuzidi.
Ngazi ya maji katika ziwa iliendelea kupanda na wakati huu kisiwa nacho kilikuwa kinatokomea haraka na maji yalikuwa yameanza kuingia katika ile pango.
Vijana hawa watajitoaje katika mkasa huu? Isitoshe, wazazi wa vijana hawa hawana habari kuhusu kilicho wapata wanao.

Comments

Hide