Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

MTO KATI YA
Hiki ni kitabu ambacho kilichapishwa na Ngugi wa Thiong'o mnamo mwaka wa 1965.
Kitabu hiki kinachambua na kuonyesha migogoro kati ya makabila asili ya Afrika na wamishonari waliokua na nia ya kueneza ukristo na kwa hivyo kusababisha kutengana kwao.
Kitabu hiki pia kina gusia matokeo ya kuishi chini ya ukoloni na pia kinaeleza kuhusu vita vya uhuru vya waafrika kutoka kwa wakoloni.
"Mto kati ya," ni kitabu ambacho kimeundwa katika vijiji viwili (Kameno na Makuyu) ambavyo ni majirani katika nchi ya Kenya.
Kameno ni kijiji ambacho kinaamini kwa kuabudu miungu mingi na kwa kulinda mila zake.
Wakaazi wa kijiji cha Makuyu wamekumbatia ukristo.
Mwingiliano na migogoro ya vijiji hivi viwili na tamaduni zao zinawasilishwa na mazoea ambayo yana idhinishwa na mandhari ambayo ni muhimu katika kitabu hiki.
Waiyaki, aliyekuwa kijana mdogo kutoka Kameno alikuwa na jukumu la kuleta pamoja vijiji hivi vya Kameno na Makuyu kwa uchungu na sadaka kama ilivyokuwa hatima yake ya kuwa atakuwa kiongozi mkubwa kwa watu wa Kameno.
Baba yake anamshauri kusoma na kukusanya habari nyingi kadri ya uwezo wake ili aweze kuhifadhi utamaduni na aweze kuhudumia watu wake.
Ilimbidi Waiyaki kuenda kuishi na mzungu katika kambi yake ili aweze kuwa mashuhuri na mwenye ujuzi kwa kuisoma mienendo yao.
Hapa anakua mtukufu na mwenye nguvu kama baba yake.
Aliweza kuanzisha taasisi ya elimu baada ya kuwa mwalimu mkuu wa shule fulani kwa madhumuni ya watu wake walioamini katika miungu mingi.
Baadaye alimpenda bintiye Joseph (aliyeongoza kijiji cha wakristo) na binti huyu aliweza kuiwacha nyumba ya baba yake ili aweze kuwa na Waiyaki.
Uungano wao unasababisha mapingamizi hivyo basi kusababisha ugumu na kuwa kizuizo kwa njia mapya ya maisha.

Comments

Hide