Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

MALKIA WA UZURI
Kitabu hiki kiliandikwa na marehemu Barbara Kimenye katika mwaka wa 1997.
Alikuwa mwandishi aliye tambulika katika kipengele cha gazeti ya Kenya ya Daily Nation.
Katika riwaya hii, marafiki wawili Adela na Keti kimzaha wanaamua kuingia katika kinyang'anyiro cha uzuri kilicho andaliwa katika kijiji chao kule Uganda.
Wasichana hawa wawili kwa bahati nzuri wanafaulu na kuendelea kwa ngazi nyengine baada ya kushinda katika kinyang'anyiro cha kwanza.
Adela ni mrembo zaidi na wathamini wake wanafanya lolote kuhakikisha kuwa wanatengeneza pesa kutokana na karama zake ambazo ni za kipekee.
Baada ya mfululizo mfupi wa vinyanganyiro vya uzuri na maonyesho, Adela anaenda jijini Nairobi na uingereza na mwishowe anatunukiwa taji la binti wa ulimwengu.
Adela anaamua kuwacha shule ili aweze kujiingiza katika kazi ya uidhinishaji wa bidhaa za uzuri wakati angali na cheo cha malkia wa uzuri mikononi mwake.
Hata hivyo,yeye ni mfungwa wa Joe ambaye ni ajenti wake.
Joe ndiye mfaidi mkuu wa mali ya Adela na pia yeye ni mwanabiashara asiye na utu.
Hakuna tofauti yoyote kati ya Joe na wamiliki wa vilabu vya siku hizi.
Furaha yao ni kuwapigisha foleni wasichana wa shule wakiwa uchi kama Malaya mbele ya wateja wao kwa malipo.
Wamiliki vilabu hawa hupenda kuwatambulisha wasichana hawa kama `bikira' kutoka Tanga, Juba, Kigali, Thailand na pengine pengi.
Wasichana hawa pamoja na Adela wanafanywa kuamini umati na kufanya dhidi ya uwezo wao tamasha zinazo hatarisha maisha yao.
Hata hivyo, Joe hayuko peke yake kwa vile ana wanawake wawili wa kando, Ujeni na Maxia ambao huandamana naye kama wasimamizi tajiri wanaogawa wanaume wazee kwa wasichana wa shule kisirisiri katika majumba makubwa na ya kibinafsi.
Maisha ya Adela yamejaa umaridadi na ndoto lakini anavyozidi kuendelea, anafanya kosa inayomtega na kufanya maisha yake yawe ya taabu.

Comments

Hide