Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Jimmy Gait
Jimmy Gait ni msanii aliyevuma sana katika nyimbo za kiinjila nchini Kenya.
Majina yake kamili ni James Ngaita Ngigi lakini yeye hujulikana kwa wengi kama Jimmy Gait, majina yaliyotoka kwa majina yake mawili ya kwanza.
Ametoa kanda nyingi ambazo zilipata umaarufu punde tu zilipoingia sokoni na kuchezwa sana katika vyombo vya habari na katika magari .
Kati ya nyimbo hizi ni 'muhadhara', 'huratiti', 'furifuri dance', 'appointment' miongoni mwa mingine.
Jimmy Gait amepata tuzo nyingi katika tamasha za Kisima na Groove Awards mnamo wa mwaka wa 2008.
Kando na uimbaji, yeye pia ni mhubiri na mwanzilishi wa kampeni inayojulikana kama 'make it or make it' ambayo mada yake ni kutia vijana moyo kwamba wanaweza kufanikiwa kimaisha iwapo watatia bidii ilikufikia malengo yao katika maisha licha ya changamoto wanazo kumbana nazo.
Jimmy Gait alizaliwa katika mwaka 1980 katika eneo la Lari counti ya Kiambu.
Yeye ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya watoto wanne.
Alihudhuria masomo yake katika shule ya msingi ya Escarpment na shule ya upili ya Lari.
Baadaye alijiunga na chuo cha mafunzo ya biblia cha Moffat ambapo alihitimu kwa diploma katika Biblia na Theolojia.
Jimmy Gait amelelewa katika familia ya kiwango cha chini sana na anasema alianza kama hana chochote. Lakini bidii yake na azma ya kufanikiwa katika maisha ndiyo imemfanya kufika pahali alipofika sasa, kama msanii mliyesifika nchini.
Alianza kuimba akiwa mdogo na alikuwa anashiriki sana katika mashindano ya muziki shuleni.
Kila wakati aliibuka mbora na kuwashinda wapinzani wake.
Alianza kazi ya muziki baada ya kukamilisha elimu yake katika chuo cha biblia.
Alitisha watu wengi aliposema anataka kufanya muziki sababu walitarajia afanye kazi aliyoisomea.
Yeye husema kuwa muziki wake sio wa pesa kama wasinii wengine mbali ni wito na njia ya kueneza injili kwa watu.

Comments

Hide