Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Jua Kali
Jua Kali ni mmojawapo wa wasanii maarufu nchini Kenya kwa nyimbo aina ya 'hip hop'.
Jina lake halisi ni Paul Nunda Julius lakini hujulikana kwa wengi kama Jua Kali.
Yeye hufanya maonyesho yake katika lugha ya Kiswahili na 'sheng'- lugha maarufu ambayo ni mchanganyiko wa Kiingereza na Kiswahili.
Mtindo wake wa kufoka unajulikana kama 'genge' na limempa jina lake la pili, 'mfalme wa genge.'
Aliungana na rafikiye wa utotoni, Clemo kuunda kundi linalojulikana kama Calif records ambalo amekishikilia hadi wa leo.
Kundi hili lilitia fora kote Afrika Mashariki na kuchangia pakubwa kukuza kwa hadhi yake katika sekta ya muziki.
Kwa sasa Jua Kali ni mmoja wa wasanii waliofanikiwa zaidi nchini Kenya na wanaolipwa juu zaidi kutumbuiza na kufanya matangazo ya biashara.
Jua Kali alizaliwa mnamo tarehe 12 Septemba mwaka wa 1979 katika eneo la 'Eastlands' Jijini Nairobi kwa Doreen na Daudi Owiti waliokuwa walimu.
Jua Kali alianza kufoka akiwa na umri wa miaka kumi huku akihimizwa na ndugu yake Christopher Sati, anayemtaja kama mmojawapo wa wale waliomtia changamoto pamoja na mamake.
Alianza elimu yake katika shule ya msingi ya Ainsworth na baadaye kujiiunga na shule ya upili ya Jamhuri na hatimaye taasisi ya kiwanda cha KCIT alikotunukiwa shahada ya diploma katika somo ya kompyuta yani Information Technology.
Mapema katika maisha yake, aliimba katika bendi ya 'Sitafuti' lakini ilisambaratika muda mfupi baada ya kuanzishwa.
Jua Kali ameandika nyimbo kadhaa zikiwemo 'Ruka', 'Nipe asali', 'kamata dame' na 'Kwaheri' ambayo ilitia fora sana kote nchini.
Jua kali pia ameshinda tuzo kadhaa katika muziki kama vile 'Chaguo La Teeniez', tuzo za Muziki za Kisima miongoni mwa mingine.
Mbali na kuimba yeye pia amekuwa akishiriki katika matangazo kadhaa ya biashara kama vile ya motorolla, Telkom, Pilsner na protex.

Comments

Hide