Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

John De Mathew
John Ng'ang'a ambaye anajulikana kwa mashabiki wake kama John De Mathew alizaliwa na kupata masomo yake katika mkoa wa kati,nchini Kenya.
Yeye ni mwimbaji maarufu kwa kabila ya wakikuyu na pia muigizaji wa bendi iliyo tambulika kwa vilabu vingi.
Muziki wake ni wa kuburudisha na wa kupasha ujumbe.
Midundo katika miziki yake ni ya kuvutia.
John ni mshairi wa kipekee kama inavyoonekana katika utungaji wake wa kuunganisha maadili ya jamii na mifumo.
Yeye hutumia methali kuelemisha jamii kwa urahisi.
Alianza kazi ya uwimbaji akiwa kijana huku akiongozwa na kutiwa changa moto na mwimbaji mkuu wa enzi hiyo, Bwana Kamaru wa jamii ya wakikuyu.
Alifuata nyayo zake hadi alipoweza kujimudu.
Msanii huyu maarufu wa jamii ya wakikuyu alishtakiwa dhidi ya misemo ya chuki.
Kamati kuu ya mshikamano na ushirikiano ilialamisha moja ya wimbo wake kama msemo wa chuki na hivi sasa anachunguzwa.
Kabla ya hatua yoyote kuchukuliwa, ilibidi wimbo wake upitishwe kwa mtafsiri aliyeithinishwa ili kuhakikisha ubayana.
Wimbo uliokuwa ukifanyiwa uchunguzi ni 'mwaka wa fisi'.
Ilisemekana kuwa wimbo huu ulikua unamtania mheshimiwa Raila Odinga aliyekuwa anawania kiti cha urais katika uchaguzi uliopita.
Wimbo huu ulipigwa marufuku na ulifaa usipeperushwe hata kidogo kwa stesheni yoyote ya redio.
Tume ya vyombo vya habari pamoja na NCIC waliweka mikakati kuchunguza stesheni zote zinazocheza wimbo wake ili kuchukuliwa hatua kali.
Pia, inadaiwa kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na mwakilishi mmoja wa akinamama kutoka mkoa wa kati na kupata mtoto naye.
Anaamini kuwa muziki unapaswa kuzingatia matukio kamili maishani na yanayonufaisha jamii kwa ujumla.

Comments

Hide