Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Joseph Kamaru
Joseph Kamaru ni mwana muziki wa Benga kutoka sehemu ya kati ya Kenya.
Alizaliwa mwaka 1939 katika jamii ya wakikuyu kule Kangema kaunti ya Murang’a.
Awali, Kamaru alikuwa msaadizi wa nyumbani mjini Nairobi.
Alipata kazi hii mwaka wa 1957.
Baadaye katika mwaka 1965, Joseph Kamaru alianza kazi ya muziki na tangu wakati huo, ameuza karibu nusu milioni ya rekodi zake.
Wimbo wa Mwangi Gachau ulimpea motisha wa kufikiria kuwa anaweza kufanya vyema zaidi yake.
Mnamo wa mwaka wa 1967, wimbo wake wa `Celina ' ulivuma sana na kumfanya kupenya katika muziki.
Yeye ndiye mwanamuziki wa kwanza Kenya kuwa na maonyesho Carnivore.
Hivi ndivyo alivyofungulia wanawaziki wengine wa wakenya lango la kuonyesha Carnivore.
Kazi yake ilifikia kilele kati ya mwaka 1975 na 1985.
Nyimbo zake zilikuwa za kisiasa na uhusiano wake na rais wa wakati huo, rais Jomo Kenyatta ulikuwa imara na wa karibu.
Baada ya kifo cha Yosia Mwangi Kariuki, Kamaru alikashifu kifo hicho na hili lilihofisha uhusiano wake wa karibu na Kenyatta.
Ujasiri wake ulirejeshwa mwaka wa 1980 na rais wa pili wa Kenya, Bwana Moi.
Alikuwa miongoni mwa walioandamana na rais Moi nchini Japani.
Kamaru aliunga mkono serikali ya viama mbalimbali jambo ambalo lilimkasirisha rais.
Baadaye katika mwaka wa 1993, Kamaru aligeukia muziki wa injili na kuliacha kundi lake liitwalo ‘Kamaru supersounds.’
Hili iliathiri umaarufu wake.
Hata hivyo, hakujutia uamuzi wake.
Yeye ni mwenyekiti wa Chama cha Kenya cha Viwanda vya senturi.
Pia, anamiliki huduma ya kanisa mjini Nairobi, ambako ana maduka ya rekodi mbili.

Comments

Hide