Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Jaguar
Charles Njagua Kanyi ni mwanamuziki wa Kenya anayejulikana kwa wengi kama Jaguar.
Yeye ni stadi kwa kufoka kiasi ya kwamba hawezi kosa kutambulika anapoigiza.
Alianza kazi ya muziki hapo awali na wimbo wa kwanza alioimba pekee ni 'Utaweza Kweli?'.
Nyimbo nyingine zake ni kama vile 'Kigeugeu', 'Fanya Mambo', 'Nikusikize', 'Nimetoka Mbali', 'Nimevuma', 'Tayari' na 'Unawasha'.
Aliutoa wimbo 'Kigeugeu' mwaka wa 2011 na bado anafurahia mafanikio yake hadi leo.
'Kigeugeu' ni video yake inayotazamwa sana hapa Kenya.
Hata hivyo, Jaguar ana utata mwingi unaomzingira, na anaugumu wa kujitoa katika utata huo.
Ili kukabiliana nao, aliitoa video ya kazi ya fadhila katika kaunti ya Turkana.
Katika video hii, alionekana akichangia wakaazi wa kaunti ya Turkana chakula.
Jaguar amefanya maonyesho yake Nairobi na Minnesota.
Pia, ameshinda tuzo kadhaa ikiwamo msanii bora wa kiume wa mwaka 2011 katika Shanga la Tuzo la Muziki la Afrika, msanii bora wa muziki aina ya boomba wa mwaka wa 2011 katika tuzo la Kisima; tena, alikuwa mmoja wapo wa wasanii bora wa kiume mwaka wa 2011 katika kitengo cha rika.
Hata hivyo,video ya 'Kigeugeu' ndiyo imeshinda tuzo nyingi.
Mbali ya kuwa mwanamuziki, Jaguar ni mwanabiashara, na alitajwa miongoni mwa wanamuziki tajiri sana nchini Kenya.
Yeye anamiliki msafara wa magari yanayojulikana kama 'Jagz cabs' na pia anamiliki karakana katika eneo ya viwanda, jijini Nairobi.
Pia, anamiliki nyumba yenye thamana ya milioni kumi na tano na magari manne yenye thamana ya milioni ishirini.
Yeye hupata angalau shillingi elfu mia tatu katika monyesho yake ya muziki.
Aidha, Jaguar anamiliki magari kadhaa ya usafiri kwa umma yanayotumika katika njia kadhaa mjini Nairobi.
Isitoshe, anamiliki kampuni ya usalama.

Comments

Hide