Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Makumbusho ya kitaifa cha Nairobi
Makumbusho ya kitaifa cha Nairobi hupatikana katika mlima makumbusho, kilomita chache kutoka jijini Nairobi. Ulijengwa mnamo wa mwaka wa 1929 kusherehekea mkusanyiko wa historia ya Kenya, utamaduni asili, na sanaa. Makumbusho haya hutafsiri urithi wa Kenya na huwapa wageni nafasi ya kusampuli urithi wa Kenya katika elimu na burudani. Awali, makumbusho haya yalikuwa katika jengo la sasa ya Nyayo ambayo baadaye ilikuwa ndogo na jengo kubwa likajengwa katika hoteli ya sasa ya Serena. Baadaye, serikali ilitenga ardhi kwa ajili ya ujenzi wake. Makumbusho haya huwavutia wageni kutoka kote duniani. Pia yanajulikana kama ukumbi wa matukio maalum, warsha na makongamano. Mbeleni, makumbusho haya yalijulikana kama makumbusho ya Coryndon lakini baadaye yaliitwa makumbusho ya kitaifa cha Nairobi. Mnamo Oktoba 15, 2005, Makumbusho haya yalifungwa milango kwa umma kwa muda mfupi, kwa ajili ya ujenzi wa miaka miwili mpaka Desemba, 2007. Jumba jipya la utawala wa makumbusho haya yalijengwa kama mojawapo ya maendeleo. Upanuzi kabambe na mpango wa uboreshaji ulinuiwa kuboresha uso wa makumbusho haya na kuyafanya mahali pa kutembelewa na watu dunia mzima. Huu ulikuwa ukarabati wa kwanza tangu mwaka wa 1930. Maria Leaky aliyatumia makumbusho haya kuifanya kazi yake mpaka mwaka wa 1961. Makumbusho haya hujumlisha maonyesho ya muda na ya kudumu ili kuhakikisha yanabaki kuwa ya kuvutia. Pia, kuna maeneo mengine yanayovutia ndani ya misingi ya makumbusho ambayo ni pamoja na; mbuga la nyoka, shamba la botaniki na alama asili. Hizi pia huvutia idadi kubwa ya wageni. Mrengo wa kibiashara wa makumbusho haya huwa na mikahawa na maduka ili kupafanya mahali pa kukumbukwa na kufurahisha.

Comments

Hide