Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hifadhi la ndege la Ziwa Nakuru
Hifadhi la ndege la ziwa Nakuru hupatikana katika mbuga la wanyama la ziwa Nakuru. Mbuga la Nakuru lilifanywa hifadhi la ndege katika mwaka wa 1960. Lengo kubwa lilikuwa kulinda kundi kubwa la heroe ambalo hupatikana hapa. Kuna zaidi ya milioni moja ya heroe katika hifadhi la ziwa hili ambalo hutokezea katika pwani. Hii hufanya pwani kuonekana kama mkeka wa waridi ulioelea. Hifadhi hili lina upana wa kilomita wa mraba 180 na hali ya hewa ni kati ya baridi na joto na unyevunyevu. Vipindi vya kuanzia Machi hadi Mei na kutoka Oktoba hadi Desemba kawaida huwa na mvua. Ni bora kuwatazama ndege kutoka jiwe la nyani na pia mlima simba. Hata hivyo, idadi ya ndege katika hifadhi hili hubadilika kutegemea idadi ya chakula. Kuna mito mitatu ambayo huleta maji katika ziwa hili nazo ni; Njoro, Makalia na Enderit. Ziwa hili lina maji ya chumvi. Ndege hawa hula mwani ambao hupatikana kwa wingi katika ziwa hili kwa sababu ya maji yake yenye joto. Wanasayansi wamegundua kwamba idadi ya heroe katika Ziwa la Nakuru hula kilo 250,000 za mwani kwa hekta ya eneo hili kwa mwaka. Hivi karibuni, idadi ya heroe katika ziwa hili imekuwa ikipungua. Hii ni kwasababu ya kuongezeka kwa utalii na uchafu kutoka kwa viwanda jirani ambavyo hutupa taka ndani ya maji. Sababu lingine ni mabadiliko katika ubora wa maji. Mabadiliko haya huharibu makao. Kawaida, ziwa hupungua wakati wa msimu wa ukame na hufurika wakati wa mvua. Pia, uchafuzi na ukame huharibu chakula cha heroe. Hii huleta wasiwasi kwani uhamaji wa heroe na vifo vinaweza kuathiri vibaya sekta ya utalii.

Comments

Hide