Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Kuja kuzaliwa
Hiki kitabu cha kuvutia kimeandikwa na Marjorie Oludhe Macgoye mzaliwa wa uingereza ambaye amekuwa mkazi wa nchi ya Kenya kwa muda mrefu.
Wahusika wakuu katika hii hadithi ni Martin na mkewe Paulina ambao wamefunga ndoa hivi karibuni.
Katika mwanzo wa hadithi, Paulina ambaye ana umri wa miaka 16 ni mjamzito.
Anasafiri kutoka kijijini hadi mji mkuu wa Nairobi kujiunga na mumewe anayeishi na kufanya kazi Kariokor.
Inatokea kwamba baada ya siku chache, Paulina anakuwa mgonjwa na kupelekwa katika hospitali ya pumwani.
Kwa bahati mbaya ile mimba inatoka.
Analazwa hospitalini lakini siku ya pili anaamua kutoka na kuelekea nyumbani bila kumngojea mumewe.
Kwa bahati mbaya anapotea njia na kwasababu hafanikiwi kufika nyumbani, inamlazimu aishi nje kwa siku mbili.
Hatimaye, Martin anampata lakini amekasirika kwavile Paulina hakumngojea.
Usiku huo na kwa mara ya kwanza anamchapa bibiye.
Hadithi hii inaendelea na Paulina anapata mimba zingine lakini zote zinatoka kabla ya wakati wa kujifungua.
Ndoa yao inazidi kuwa ngumu, na kutofautiana pia kunaongezeka.
Martin anaanza kutokuwa mwaminifu na kuanza uhusiano na wanawake wengine.
Paulina naye anaamua kumuacha na kuelekea Kisumu.
Huko anafanikiwa kupata kazi ya uwalimu.
Naye pia anabadilisha mienendo na kuanza kuhusishana na mwanaume mwingine.
Chakushangaza ni kuwa wakati huu anafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume.
Furaha yake inakatizwa wakati mtoto huyu anauliwa na polisi wanapofyatulia umati risasi katika mji wa Kisumu.
Paulina anaamua kurudi Nairobi ambapo anaajiriwa kama mjakazi kwa tajiri mmoja ambaye yuko katika harakati za siasa.
Martin anaanza kumtembelea Paulina na wakati kitabu hiki kinamalizika wameshakuwa mume na mke tena.
Mara hii, Paulina anafanikiwa kumpa Martin mtoto.

Comments

Hide