Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Notes

Unlock In-Depth Explanations & Exclusive Takeaways with Printable Lesson Notes

Unlock Lesson Notes and Transcripts for every single lesson. Sign Up for a Free Lifetime Account and Get 7 Days of Premium Access.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Kifo Kisimani
Hiki ni kitabu cha tamthilia ambacho kimeandikwa na Kithaka wa Mberia.
Kinaelezea hadithi ya kuvutia kuhusu kisima kilicho pekee katika kijiji cha Butangi na chifu anayeitwa Bonoko.
Bonoko amekataza watu kuteka maji kwenye kisima hiki.
Riwaya inaanza kwa mkutano unaopaswa kuanza lakini watu hawajaonekana.
Vibaraka wake chifu wanatayarisha sehemu ya mkutano kwa kupanga viti.
Inakisiwa kuwa Mwelusi, kijana mmoja ambaye haambatani na uongozi wake Bonoko ndiye aliye wachochea watu wasihudhurie ule mkutano.
Chifu Bokono anajawa na mawazo huku akihofia kuwa utawala wake uhatarini.
Mkewe Nyalwe anamsihi abadilishe namna anavyoongoza kwavile hapendwi na watu kwani wafuasi wake wamekuwa wakimdanganya.
Mwelusi anashikwa na kupelekwa gerezani ambapo anateswa na askari.
Nia yao ni kumfanya Mwelusi akiri kuwa yeye ndiye kiongozi wa mapinduzi dhidi ya Bonoko na kwamba atubu mbele yake chifu akiwa anataka kuwekwa huru.
Lakini Mwelusi anakana jambo hilo kabisa.
Atega anamtembelea Mwelusi gerezani na kumpelekea mkate na mvinyo ambao askari wanachukua.
Mwelusi anatumia tupa iliyokuwa ndani ya mkate kukata minyororo na kufaulu kutoroka gerezani.
Nduguye Genge anadanganywa kwa kuahidiwa kuwa atamwoza binti wa chifu iwapo atamuua Mwelusi.
Anamfanyia hila kwa kumwambia kuwa amebadilisha fikira zake na kuwa anamuunga.
Anamwambia Mwelusi kuwa anasiri kutoka kwa mamake anayotakakumweleza.
Mwelusi anamfuata katika chumba cha siri ambapo anamuua.
Hadithi inapoisha,watu wameungana kupinga uongozi wa Bonoko.
Wanamshika pamoja na vibarua wake na kuwaweka kwenye uja. Tangu hapa wanaweza kuleta mageuzi katika uongozi wa Butangi.

Comments

Hide