Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya kusherehekea utamaduni wa jamii ya wamaasai ni siku ambayo ilianzishwa ili kuhifadhi utamaduni wao pamoja na wanyama na mimea wa mwituni. Siku hii inasherehekewa mwezi wa nane ama mwezi wa tisa.
Video hii inatoa elimu kuhusu jinsi sikukuu hii husherehekewa.
Je, unajua ni kwa nini jamii ya kimaasai ni ya kipekee nchini Kenya hasa katika nyakati hizi?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Tukio hili hufanyika katika kiwanja cha enzi za kabla ya historia cha Olorgesailie. Waandalizi wakuu ni kundi la ACC na lile la SORALO ambayo ni makundi inayohusika na uhifadhi. Wazee hubariki ardhi na mifugo ya wamaasai. Wanawake huimba na kucheza nyimbo za kitamaduni na baadaye kutoa mizigo juu ya punda kama ilivyo desturi. Mizigo hii huwa ni chakula na bidhaa za kitamaduni, vitu ambazo hutumika kwa sherehe hizi.
Hotuba hutolewa na washika ndao tofauti kama wawakilishi wa makundi ya uhifadhi, mwakilishi wa chumba cha kitaifa cha kuhifadhi vitu vya kale ili watu waone, waziri anayesimamia wizara ya mila, desturi na utamaduni na pia kutoka kwa wageni wengine mashuhuri.
Vijana wa enzi za kisasa hufundishwa jinsi utamaduni wa kimaasai ulifanyika na ustadi wake. Wao pia hupata elimu muhimu kuhusu uhifadhi wa mila na desturi. Wao hufunzwa jinsi masomo haya inawasaidia kwa sasa na kwa siku za usoni hasa kwa utalii wa ndani na pia utalii wa kimataifa.
Chumba cha kuhifadhi utamaduni wa kimaasai cha kuingiana kinachojengwa katika eneo la Olorgesailie kitakuwa kinaonyesha mila hizi na desturi kwa mwaka mzima na kwa hivyo sikukuu hii itakuwa ya ukumbusho tu na sherehe maalum.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ni kwa nini jamii ya wamaasai ni ya kipekee nchini Kenya hasa katika nyakati hizi?
Jamii ya kimaasai nchini Kenya wameweza kuhifadhi na kudumisha mila, desturi na tamaduni zao hata ingawa hizi ni nyakati ambazo jamii nyingi zinapoteza tamaduni zao na kukumbatia ustaarabu.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, jamii katika nchi yako huhifadhi mila na desturi kivipi?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide