Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya Jamhuri husherehekewa tarehe 12 mwezi wa kumi na mbili. Ni ukumbusho wa wakati Kenya ilipata uhuru na kuwa nchi huru, kutoka kwa utawala wa waingereza.
video hii itatupa elimu kuhusu jinsi wananchi wa kenya husherehekea sikukuu hii.
Je, nchi kuwa jamhuri inamaana gani na Kenya ilikuwa nini kabla ya kuwa jamhuri?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Tarehe kumi na mbili Desemba wakenya huungana pamoja na kuanza na kuimba wimbo wa taifa. Gwaride la askari huchezwa kuwateremesha Rais na wageni wote ambao huhudhuria. Wafanyikazi wa serikali huvaa mavazi rasmi inayoambatana na vitengo zao za kazi.
Hotuba za kisiasa hutolewa kuanzia kwa wawakilishi wa majimbo, naibu wa Rais na mwishowe Rais wa Kenya. Wasemaji wote huongea na kuwapongeza waliopigania uhuru haswa Dedan Kimathi ambaye aliteswa na kunyongwa kwa ukakamavu wake na kuhusika kwa harakati za kutafuta uhuru.
Wakenya husherehekea uhuru kwa nyimbo za kitamaduni zilizoimbwa wakati wa uasi wa MAU MAU. Mashairi, nyimbo na kucheza ngoma huwaelimisha vijana kuhusu historia ya Jamhuri ya Kenya. Baada ya mkutano wa hadhara watu huenda kuona sinema zinazohusu uhuru wa Kenya kwa nyumba zao au kwa vyumba za sinema huku wakila chakula wakipendacho cha nyama choma na kunywa pombe.
Sikukuu hii ni marudufu kwa vile inasherehekea wakati Kenya ilipata jamhuri mwaka wa Decemba 12, 1964 na kuungana na nchi zingine zisizokuwa na wafalme. Pia, ni wakati Kenya ilipata uhuru kamili kutoka kwa waingereza mnamo wa mwaka wa Decemba 12, 1963.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, nchi kuwa Jamhuri inamaana gani? Kenya ilikuwa nini kabla ya kuwa jamhuri?
Nchi ya Kenya sasa ni Jamhuri ya Kenya kwa sababu iliacha kutawaliwa na wakoloni na sasa hutawaliwa na viongozi wakenya ambao huchaguliwa na watu kwa njia ya kidemokrasia. Hapo awali Kenya ilikuwa chini ya himaya ya Uingereza.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, nchi yako ishawahi kutawaliwa na nchi ingine?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide