Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Katika mwezi wa Ramadan, Waislamu kote duniani hufunga kukula na kukunywa ili kuhusika na vitendo vya kupeana na kudumisha amani. Huu ni wakati wa kufanya upya maisha ya kiroho. Mwisho wa Ramadan, waislamu husherehekea kufungua kukula na kukunywa katika sikukuu ya Eid al-Fitr.
Katika fundisho hii utajua jinsi waislamu nchini Kenya husherehekea sikukuu ya mwisho wa Ramadan
Je, unajua ya kwamba tarehe ya mwaka wa kusherehekea Eid inategemea jambo ipi?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Waislamu hupeana kiasi fulani ya chakula, mavazi, na pesa kwa wanyonge katika jamii. Wao husherehekea na jamaa na marafiki mwishoni mwa mwezi kwa baraka na furaha. Chakula kinachopatikana kwa wingi ni mchele, shayiri na tende ili kuhakikisha ya kwamba maskini hohehahe pia wanachakula cha kusherehekea sikukuu hii. Zawadi hizi huitwa sadaqah al-fitr.
Wakati wa sikukuu ya Eid al-Fitr waislamu huungana pamoja asubuhi na mapema mahali wazi kama vile kwa viwanja ama kwa misikiti na kufanya maombi ya Eid al-Fitr. Ibada hii inahusu mahubiri pamoja na maombi mafupi ya wafuasi wa kiislamu ambayo huongozwa na Imam.
Baada ya ibada ya Eid, waislamu hutawanyika na kuwatembelea familia na marafiki. Wao hupeana zawadi haswa kwa watoto wachanga. Watu hupiga simu kwa jamaa walio mbali ili kuwatakia sikukuu ya Eid yenye fanaka. Kama ilivyo desturi, sherehe hizi huendelea kwa siku tatu lakini nchini Kenya, siku moja tu ndio sikukuu rasmi ya kiserikali.
Kitindamlo kikuu cha Eid nchini Kenya ni pudini ambayo imetengenezwa na wali ambao umefanywa uwe mtamu kwa kutumia maziwa. Vitindamlo vingine ni kama biskuti, vitobosha, keki na hata switi za nazi.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ya kwamba tarehe ya mwaka wa kusherehekea Eid inategemea jambo lipi?
Tarehe ya kusherehekea Eid inategemea kuonekana kwa mwezi mpya. Waislamu hungoja kuona mwezi ama matangazo kutoka Mecca. Watu wengine hutabiri tarehe kwa kutumia hesabu ya nyota au elimu ya nyota.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, sikukuu hii inasherehekewa nchini mwako? Kama ndio, inasherehekewa kwa siku ngapi kama sikukuu rasmi?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide