Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya Mama Mzazi husherehekewa tarehe tofauti kila mwaka. Kwa mfano, katika mwaka wa 2014 ilikuwa tarehe ya Mei 11. Kila mtoto kote duniani humtambua mama yake na kuchukua fursa hii kumshukuru kwa kazi njema ya kumzaa na kumlea.
Katika video hii utajua jinsi Wakenya huendesha sherehe hii ya Sikukuu ya Mama Mzazi.
Je, unajua ni mwanamke au mama yupi alituzwa zawadi ya utendaji wema na kuleta amani hapa nchini Kenya?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Nchini Kenya, sala maalum hufanyika kwa makanisa ama misikiti kwa heshima ya kina mama. Wamama pia husherehekewa kwa kuletewa kiamsha kinywa kwa kitanda. Mama huruhusiwa kulala hadi macheo. Watoto pamoja na baba yao humtayarishia mama kiamsha kinywa akipendacho kama vile keki, kuki, chapati ya mseto wa nyanya ama bokoboko pamoja na chai, uji ama maji ya matunda.
Watoto humnunulia ama kumtengenezea maua ya kupendeza. Watoto wachanga hujikakamua na kutengeneza kadi siku moja kabla ya sikukuu hii. Watoto wakubwa huonelea heri kununua kadi, nguo, mapambo ama zawadi zingine za kumpongeza mamao kutoka kwa maduka. Watoto wakubwa huwapangia mama zao kutembelea behewa la starehe na kuwarembesha kweli kweli kwa vile huwa hawana wakati wa kijistarehesha na hata kurembeka.
Baadhi ya wakenya huamua kuenda kwa mandari kama familia. Wao hufanya michezo na mambo ambayo humfanya mama kujisikia wa maana na wa kipekee. Baba na watoto huhakikisha ya kwamba mama hafanyi kazi yeyote haswa kazi ya nyumba. Wao hutayarisha chakula cha jioni na kufanya usafi wa nyumbani. Wengine huona heri kumpeleka kula nje kwa mkahawa.
Kama vile Sikukuu ya Wapendanao sikukuu hii husherehekea mapenzi kati ya watu wawili wapendanao, kama vile bibi na bwana. Sikukuu ya Mama Mzazi husherehekewa na kuonyesha mapenzi kwa mama.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ni mwanamke au mama yupi alituzwa tuzo la kuleta amani hapa nchini Kenya?
Mwaka wa 2004, Profesa Wangari Maathai alikuwa mwanamke wa kwanza barani Afrika kupokea tuzo la kuleta amani. Alisimama na kudumisha maendeleo, demokrasia na amani.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, kuna tofauti yeyote jinsi wakenya husherehekea Sikukuu ya Mama Mzazi na vile nyinyi husherehekea?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide