Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya Krismasi inasherehekewa mnamo tarehe 25 (ishirini na tano) Desemba (mwezi wa kumi na mbili) kila mwaka. Wakristo kote duniani huungana makanisani kwa mkesha wa Krismasi ambao ni tarehe 24 Desemba na kugonja itimie saa sita kamili muda ambao waumini huamini Yesu Kristo alizaliwa.
Funzo hili lita tuangazia jinsi wakristo wa Kenya husherekea sikukuu ya Krismasi.
Je, unajua ikiwa watu husafiri au vile jinsi watu wa jijini husherehekea sikukuu ya Krisimasi?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Sikukuu ya Krismasi huanza tarehe 24. Wafanyakazi wengi hupewa likizo kuanzia tarehe 23 ili wajiandae vilivyo kwa siku ya tarehe 25 ambayo ndio siku ya maana sana. Mchana wa mkesha wa Krisimasi watu hununua bidhaa zote watakazohitaji katika maduka ya kijumla na kwingineko. Chakula kama unga, mchele, vinywaji na zawadi tofauti hununuliwa sana. Hii ni kwa sababu ni duka chache sana ambazo hufunguliwa siku hii kuu. Wafanya biashara huchukua fursa hii kuuza vitu vingi sana kwa bei nafuu.
Mkesha wa Krisimasi wakristo wengi huwa hawalali. Wao hungoja saa sita kamili za usiku itimie kwa vile ni wakati ambao waumini wengi huamini ni wakati Yesu Kristo alizaliwa. Wengi huamua kungojea nje watakapo weza kutazama mwezi juu angani. Wakiwa nje wao huwasha moto na kuimba nyimbo za kumtukuza Yesu. Wengine huenda kanisani na kushirikiana na watoto wakiimba na kuigiza michezo inayohusu na kuzaliza kwa Kristo.
Siku kuu ya Krismasi, tarehe 25 ifikapo watu husherehekea kwa njia tofauti. Watu wengi huenda kanisani masaa ya asubuhi na kurudi kusherehekea kwa mlo na vinywaji vya vipekee. Wakenya wengi hupenda nyama ya mbuzi iliyochomwa. Walio mbali na nyumbani katika mikahawa ya kifahari huandaliwa chakula maalum wakipendacho. Watu wanapomaliza kula na kunywa hupanga kutembelea pahala kama mbuga la wanyama, kuogelea na pahala pa kuwafurahisha watoto hadi machweo. Watoto wengi huwa wamevalia mavazi mapya na yakupendeza.
Watu hutumia fedha zao kwa anasa, na hata kusahau kuweka akiba kwa ajili ya kujikimu kimaisha na kupata riziki baada ya sikukuu ya Krisimasi. Sikukuu hii watu hufanya chochote kuwafurahisha jamii na marafiki.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ikiwa watu husafiri au vile jinsi watu wa jijini husherehekea sikukuu ya Krisimasi?
Watu hupenda kusafiri wakati wa likizo wa Krisimasi kutoka kwa miji wanamoishi. Wao huenda mashambani waliko na asili ama huko Mombasa, Naivasha ama katika mikahawa ya mbali kama vile Mkahawa wa mlima Kenya.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je sikukuu ya Krisimasi huwapea watu wa nchi yako msisimuko wa furaha kama inavyowapa watu wa kenya?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide