Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Wakenya husherehekea wiki ya mitindo ya nguo kwa kuonyesha mitindo mizuri kutoka kwa michoro ya kisasa na ya kitamaduni. Mitindo hii huundwa na wachoraji wabunifu ambao huchukua fursa hii kuonyesha ubunifu wao. Waandalizi hubadilisha tarehe za tamasha hii kila mwaka.
Katika video hii utajua jinsi wakenya husherehekea wiki ya mitindo.
Je, Unajua tukio hili limekuwa na majina ngani?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Tukio hili ambalo hufanyika jijini Nairobi huwapea nafasi waundaji wa mitindo kutoka Kenya na nchi za kigeni kutakabari mikusanyiko mipya ya mitindo kwa njia ya maonyesho. Wanunuzi na wanahabari hukagua mitindo hii na kuitafutia soko. Wakati huu ndio watu hujua ni mitindo upi uko kwa nyakati Fulani.
Katika wiki ya mitindo nchini Kenya, matendo yanayohusika na waundaji halisi wa hapa nchini na wa kimataifa hufanyika. Anwani za hali ya juu, wafadhili na wanahabari hufuata kwa makini kila kitu kinachoendelea kwa tukio hili. Wafadhili sana sana huwa na alama ya biashara ya mashirika makubwa ya kimataifa.
Chakula cha jioni cha mkeka mwekundu huandaliwa na karamu ya kufana mno hufanyika. Wakati huu waundaji wa mitindo hupata anwani za wanunuzi au watu wanaoweza kuiinua kibiashara. Waliohudhuria hupata burudani na maonyesho ya bidhaa na huduma za kifahari za kuinua maisha.
Sikukuu hii huwa na nia ya kuifanya Kenya kuwa mji mkuu wa mitindo ya kimaisha barani Afrika. Watu wanaotaka kuinua biashara ya waundaji wa Kenya hufanikiwa kwa vile mashindano haya ni mbunifu.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, Unajua tukio hili limekuwa na majina yapi?
Wiki ya mitindo ya Kenya ilianza kwa majina tofauti. Kwanza ilikuwa ikiitwa sherehe ya mwelekeo wa mitindo ya Kenya, ikaitwa tukio linalopendwa sana la mitindo katika sehemu ndogo ya Sahara barani Afrika halafu ikaitwa mtoto wa akili ya Sonu Sharma na sasa hivi inaitwa wiki ya mitindo ya Kenya.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, kuna sherehe za aina hii nchini mwenu ambazo huweza kusaidia waundaji wa mitindo kupata soko na kuvutia watalii?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide