Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya wafanya kazi wa umma hufanyika tarehe moja mwezi wa tano (Mei) wa kila mwaka. Wakenya wote hupata likizo ili kusherehekea utendaji kazi yao. Sherehe huandaliwa na vyama kama vile KOTU amba kinasimamia maswala ya wafanya kazi wote nchini Kenya.
Fundisho hili linatoa funzo jinsi sherehe za sikukuu ya wafanya kazi wa umma husherehekewa.
Je unajua ni wafanya-kazi wagani nchini Kenya ambao husherehekea sikukuu hii?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Wafanyi kazi husafiri kuelekea uwanja wa Uhuru ambako sherehe hufanyiwa. Wengine huamua kukaa nyumbani na kutazama maonyesho ya sherehe hizo katika runinga zao ili kuepuka kusongamana wa watu. Sherehe huongozwa na mkurugenzi na chama cha wafanya kazi nchini (KOTU).
Tafrija ifuatayo pia hutendeka katika uwanja wa Uhuru. Wageni waheshimiwa ambao ni Rais wa Jamhuri ya Kenya, waziri wa kazi za utumishi wa umma na maafisa wakuu serikalini hutumbuizwa kwa nyimbo na michezo ya kuigiza na maonyesho mbali mbali kutoka wizara tofauti. Wanamuziki wa nyimbo za injili na pia wanao onyesha kujivunia nchi pia hutumbuiza wageni na kuonyesha vipawa vyao.
Wafanya kazi wa umma hungoja kwa shauku kuu hotuba ya Rais. Hii ni kwa sababu Rais huwaongeza mishahara pamoja na marupurupu mengine kama vile marupurupu ya nyumba, ya kusafiri na ya kuketi kwa mikutano. (Yeye huongeza mshahara hata kwa mtu anayepokea mshahara duni sanar.)
Wafanyakazi wengi wa umma hutulia kabisa hadi Rais atakapo ongea kuhusu mishahara kisha wanatawanjika baada yo hotuba.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je unajua ni wafanya kazi wagani nchini Kenya ambao husherehekea sikukuu hii?
Wafanya kazi wa kiserikali na pia wasioajiriwa na serikali hupewa likizo ili kupumzika. Hii haimaanishi ya kwamba maduka na mazahanati hufungwa mchana kutwa. Wafanyabiashara na mashirika zingine za kibinafsi hufunguliwa ingawaje kwa masaa machache.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, kuna siku maalum ambayo imetengwa kusherehekea wafanyakazi wa umma katika nchi yenyu?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide