Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya Pasaka inasherehekewa kote duniani mkiwamo nchi ya Kenya. Sikukuu hii ni ukumbusho wa kufufuka kwa Yesu Kristo siku tatu baada ya kusulubiwa kwake msalabani.
Funzo hili litakufunza jinsi Wakenya hukumbuka kufufuka kwa Yesu Kristo na jinsi wa Kenya huonyeshana ukarimu wao.
Je, unajua watu wengi hupenda kutumia muda huu na watu wagani katika jamii?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Sikukuu ya pasaka huwa siku ya Jumapili lakini huwekwa siku ya Jumatatu ili kuwezesha wanaofanya kazi kuisherehekea pamoja na jamaa na marafiki. Watu husherehekea kwa minajili ya kumuomba Yesu azaliwa tena maishani mwao. pia, ni siku ya kumwabudu Mungu kwavile Yesu Kristo aliaga dunia, na kufufuka kutoka kwa wafu na kushinda mauti.
Watu huandaa chakula maalum na kukula baada ya kufunga na kuomba wa siku ya Ijumaa Kuu. Kama inavyostahili mtu kukula baada ya kujinyima chakula, wao hula chakula chepesi kama uji, pilau, maji ya matunda ili kuwezesha mwili kusiaga vizuri. Familia za wakristo husoma bibilia pamoja na kuomba na hatimaye kula na kunywa ili kusherehekea kufufuka kwa Yesu
Pasaka ni siku ya Kikiristo lakini pia waumini na makafiri hujihusisha kwa likizo hii ili kujistarehesha. Wao hukita hema mahali tofauti kama vile Naivasha. Wakenya pia hupendelea kwenda Pwani au Mombasa na pia kwa mikahawa ya kifahari, na mbuga za wanyama. Wengine huenda kutembelea nchi za kigeni.
Mayai hutumika kwa sikukuu ya Pasaka kwa vile inaashiria mwanzo wa maisha mapya. Mayai iliyopakwa rangi hupeanwa na pia hutumika kurebesha kanisa wakati wa pasaka.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua watu wengi hupenda kutumia muda huu na watu wangani katika jamii?
Wakristo na watu wakuu serikalini, kwa uhisani mwema, huwatembelea wasio na bahati katika jamii na kuwapelekea vitu vya kuwasaidia kujikimu maishani. Nyumba za mayatima, watu wazee na wakimbizi wa ndani sana sana hubahatika kwa matendo haya.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, kuna uhusiano wowote kati ya jinsi wakristo husherehekea pasaka nchini Kenya na nchini mwenu?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide