Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Jumapili ya Mtende ni sikukuu ya kikristo inayosherehekewa juma moja kabla ya Pasaka, wakati ambapo Yesu Kristo alifufuka kutoka kwa mauti. Siku hii ni ukumbusho wa vile Yesu Kristo aliingia kwa majaribu huko Yerusalem.
Fundisho hili litaangazia jinsi wakristo nchini Kenya husherehekea Jumapili ya Mtende.
Je, wakristo hutumia matawi ya mti gani kuazimisha sherehe ya Jumapili hii?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Katika sikukuu ya Jumapili ya Mtende, waumini huamka mapema na kukusanyika mahali pamoja pateule. Wao huomba na kuanza safari ya kutembea kwa miguu wakielekea kanisani. Wanapotembea wao huimba nyimbo zinazohusika na mateso aliyopitia mwana wa mungu huku wakipeperusha matawi ya mitende.
Waumini wanapofika kanisani ibada maalum ya sikukuu hii hufanyika. Katika makanisa mengi, misalaba iliyotengenezwa na majani ya mitende hubarikiwa na wachungaji, maaskofu au makasisi halafu hupewa wafuasi. Mitende hutumika kurembesha kiingilio, kuta na paa za makanisa na kwingineko.
Pia, watoto huhusika kwa kusimulia hadithi za bibilia zinazohusika na matukio ya Jumapili ya mtende. Pia, vikundi tofauti vya kanisa huweza kuonyesha michezo, mashairi na nyimbo zinazopelekana na maelezo ya bibilia kuhusu siku hii ambayo Yesu aliingia Yerusalem akiwa juu ya Punda.
Sikukuu hii husherehekewa siku ya likizo kwa wanafunzi na wafanyikazi wote, wanaolipwa mishahara na wanaopata ajira. Idadi kubwa ya wakenya wangependelea sikukuu hii iwe Jumatatu ili wapumzike.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, wakristo hutumia matawi ya mti gani kuazimisha sherehe za Jumapili hii?
Wakristo nchini Kenya na kote duniani hutembea kwa barabara huku wakibeba matawi ya mti wa Mtende. Hii ni njia ya kuashiria jinsi watu walivyotandika mavazi yao pamoja na mitende ili Yesu apitie juu walipokuwa wakitembea na Yesu alipokuwa akiingia Yerusalemu.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, wakristo nchini mwenu huitambua sikukuu hii?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide