Kifo Kisimani |
Hiki ni kitabu cha tamthilia ambacho kimeandikwa na Kithaka wa Mberia. |
Kinaelezea hadithi ya kuvutia kuhusu kisima kilicho pekee katika kijiji cha Butangi na chifu anayeitwa Bonoko. |
Bonoko amekataza watu kuteka maji kwenye kisima hiki. |
Riwaya inaanza kwa mkutano unaopaswa kuanza lakini watu hawajaonekana. |
Vibaraka wake chifu wanatayarisha sehemu ya mkutano kwa kupanga viti. |
Inakisiwa kuwa Mwelusi, kijana mmoja ambaye haambatani na uongozi wake Bonoko ndiye aliye wachochea watu wasihudhurie ule mkutano. |
Chifu Bokono anajawa na mawazo huku akihofia kuwa utawala wake uhatarini. |
Mkewe Nyalwe anamsihi abadilishe namna anavyoongoza kwavile hapendwi na watu kwani wafuasi wake wamekuwa wakimdanganya. |
Mwelusi anashikwa na kupelekwa gerezani ambapo anateswa na askari. |
Nia yao ni kumfanya Mwelusi akiri kuwa yeye ndiye kiongozi wa mapinduzi dhidi ya Bonoko na kwamba atubu mbele yake chifu akiwa anataka kuwekwa huru. |
Lakini Mwelusi anakana jambo hilo kabisa. |
Atega anamtembelea Mwelusi gerezani na kumpelekea mkate na mvinyo ambao askari wanachukua. |
Mwelusi anatumia tupa iliyokuwa ndani ya mkate kukata minyororo na kufaulu kutoroka gerezani. |
Nduguye Genge anadanganywa kwa kuahidiwa kuwa atamwoza binti wa chifu iwapo atamuua Mwelusi. |
Anamfanyia hila kwa kumwambia kuwa amebadilisha fikira zake na kuwa anamuunga. |
Anamwambia Mwelusi kuwa anasiri kutoka kwa mamake anayotakakumweleza. |
Mwelusi anamfuata katika chumba cha siri ambapo anamuua. |
Hadithi inapoisha,watu wameungana kupinga uongozi wa Bonoko. |
Wanamshika pamoja na vibarua wake na kuwaweka kwenye uja. Tangu hapa wanaweza kuleta mageuzi katika uongozi wa Butangi. |
Comments
Hide