| KUOKOLEWA KWA HELIKOPTA |
| Kitabu hiki kimeandikwa na K W Wamitila aliyezaliwa tarehe 13 Juni mwaka wa 1965. |
| Yeye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Nairobi. |
| Hii ni hadithi inayohusu kituko kizuri ambacho baadae kilienda mrama. |
| Katika kitabu hiki, Zeke, kijana wa umri wa miaka kumi amshawishi Kate, binamu yake aliyekuja kumtembelea, ya kuwa andamane naye hadi kisiwa kilichokuwa hapo karibu. |
| Wawili hawa waliondoka na kwenda kwa kile kisiwa bila kumfahamisha yeyote. |
| Dalili ya mvua ilikuwa wazi hapo tu walipowasili ziwani. |
| Zeke anaenda mbele na kumkaribia mvuvi mmoja anayemwomba awapeleke kisiwani bila malipo. |
| Kwa mara ya kwanza, mvuvi anasita kuwapeleka kwa vile anahisi kuwa kuendesha mashua katika hali ile mbaya ya anga ingekuwa ni hatari lakini anabadili mawazo yake Zeke alipozidi kusisitiza. |
| Mvuvi anawapeleka Zeke na Kate kwenye kisiwa na kurudi kuvuvi kwa haraka baada ya kuwafikisha pale kisiwani. |
| Peke yao, vijana hawa wawili wanaanza kuvumbua kisiwa hiki ambapo wanafanikiwa kupata pango lililo kuwa ndani ya mbuyu uliofaraghiwa. |
| Waliamua kuingia ndani zaidi ya ile pango ambamo walibebeka na mazuri yaliyokuwa ndani. |
| Kulikuwemo maandishi ya kigeni, alama za kusisimua kwenye kuta na mawe meusi zilizofanya akili za vijana hawa kuduwaa na kubebeka zaidi. |
| Mvua ulianza kunyesha kwa uzito na mvuvi akaondoka kwa haraka na kusahau kuwachukua vijana hawa. |
| Alikumbuka kuhusu vijana hawa mara tu alipofika ukingoni. |
| Kurudi katika kile kisiwa ili kuwaokoa Zeke na Kate ilikuwa haiwezekani kwa vile mvua ulivyokuwa ukinyesha kwa wingi, ndivyo hali ya hatari ilivyoendelea kuzidi. |
| Ngazi ya maji katika ziwa iliendelea kupanda na wakati huu kisiwa nacho kilikuwa kinatokomea haraka na maji yalikuwa yameanza kuingia katika ile pango. |
| Vijana hawa watajitoaje katika mkasa huu? Isitoshe, wazazi wa vijana hawa hawana habari kuhusu kilicho wapata wanao. |
Comments
Hide