| KUNRADHI! NDOTO LAKO LAKUITA | 
                                                                
                                                                            | Kitabu hiki kimeandikwa na Mbugua Mumbi ambaye ana shahada ya diploma katika somo la benki na hitimu zaidi katika diploma ya  somo la uuzaji. | 
                                                                
                                                                            | Sasa anaendeleza masomo yake katika usimamizi kimkakati wa biashara katika chuo kikuu cha Leicester kule Uingereza. | 
                                                                
                                                                            | Kitabu hiki kinakupa mbinu ya kisayansi ya kufikia kiwango chochote cha mafanikio ambacho unaweza taka. | 
                                                                
                                                                            | Kanuni zilizo onyeshwa hapa ni muhimu na lugha iliyotumika ni wazi ikiwa pamoja na mazoezi ya kusaidia  kufahamu kwa ukamilifu matumizi yake. | 
                                                                
                                                                            | Binadamu anafaa kujua ukweli kujihusu. | 
                                                                
                                                                            | Kila binadamu ana hamu ya kuhitimu. | 
                                                                
                                                                            | Hakuna mwanadamu angelipenda kutia bidii kwa mpango ilikutofaulu. | 
                                                                
                                                                            | Hakuna kitu chochote kinaweza kupatikana bila kuhusisha mbinu kadhaa. | 
                                                                
                                                                            | Ili jambo lolote liweze kufaulu, ni lazima sheria kadhaa ziweze kuhusishwa. | 
                                                                
                                                                            | Sheria hizi ndizo ufunguo mkubwa katika kuhitimu na kuelewa matumizi yake ni hakikisho ya maisha bora unayotarajia. | 
                                                                
                                                                            | Ujumbe ulio katika kitabu hiki inabadilisha na kuokoa maisha. | 
                                                                
                                                                            | Njia ya kipekee ya ufunulizi uliyotumika inaunganisha hotuba na zoezi ya kibinafsi unao waweka watu kwenye safari inayopendeza ya kufaulu na yenye furaha. | 
                                                                
                                                                            | Msingi wa kitabu hiki ni ukweli mtupu na kinaelezea uwezo mwingi ulimondani ya binadamu lakini hautumiki. | 
                                                                
                                                                            | Kitabu hiki pia kitakufunza na kukusaidia kujigundua na kile ulicho nacho ili uweze kuishi maisha unayo tamani. | 
                                                                
                                                                            | Kinafunza jinsi ya kufanya kazi kwa njia kadhaa kwa kuelezea jinsi ya kutumia akili na jinsi ya kuelewa maumbile. | 
                                                                
                                                                            | Kitabu hiki kina vitendo na vilevile kina mafunzo. | 
                                                                
                                                                            | Utagundua mambo yanayotia moyo na ya kushangaza. | 
                                                                
                                                                            | Kupitia kitabu hiki, unauwezo wa kubadilisha na kuokoa maisha yako. | 
                                                                
                                                                            | Utagundua ya kuwa yote yamo katika uwezo wako. | 
                                                        
                     
Comments
Hide