| KUNRADHI! NDOTO LAKO LAKUITA |
| Kitabu hiki kimeandikwa na Mbugua Mumbi ambaye ana shahada ya diploma katika somo la benki na hitimu zaidi katika diploma ya somo la uuzaji. |
| Sasa anaendeleza masomo yake katika usimamizi kimkakati wa biashara katika chuo kikuu cha Leicester kule Uingereza. |
| Kitabu hiki kinakupa mbinu ya kisayansi ya kufikia kiwango chochote cha mafanikio ambacho unaweza taka. |
| Kanuni zilizo onyeshwa hapa ni muhimu na lugha iliyotumika ni wazi ikiwa pamoja na mazoezi ya kusaidia kufahamu kwa ukamilifu matumizi yake. |
| Binadamu anafaa kujua ukweli kujihusu. |
| Kila binadamu ana hamu ya kuhitimu. |
| Hakuna mwanadamu angelipenda kutia bidii kwa mpango ilikutofaulu. |
| Hakuna kitu chochote kinaweza kupatikana bila kuhusisha mbinu kadhaa. |
| Ili jambo lolote liweze kufaulu, ni lazima sheria kadhaa ziweze kuhusishwa. |
| Sheria hizi ndizo ufunguo mkubwa katika kuhitimu na kuelewa matumizi yake ni hakikisho ya maisha bora unayotarajia. |
| Ujumbe ulio katika kitabu hiki inabadilisha na kuokoa maisha. |
| Njia ya kipekee ya ufunulizi uliyotumika inaunganisha hotuba na zoezi ya kibinafsi unao waweka watu kwenye safari inayopendeza ya kufaulu na yenye furaha. |
| Msingi wa kitabu hiki ni ukweli mtupu na kinaelezea uwezo mwingi ulimondani ya binadamu lakini hautumiki. |
| Kitabu hiki pia kitakufunza na kukusaidia kujigundua na kile ulicho nacho ili uweze kuishi maisha unayo tamani. |
| Kinafunza jinsi ya kufanya kazi kwa njia kadhaa kwa kuelezea jinsi ya kutumia akili na jinsi ya kuelewa maumbile. |
| Kitabu hiki kina vitendo na vilevile kina mafunzo. |
| Utagundua mambo yanayotia moyo na ya kushangaza. |
| Kupitia kitabu hiki, unauwezo wa kubadilisha na kuokoa maisha yako. |
| Utagundua ya kuwa yote yamo katika uwezo wako. |
Comments
Hide