| Ken wa Maria |
| Ken wa Maria anafanya muziki wake katika lugha ya kikamba. |
| kwa sasa yeye ndiye msanii mmaarufu kutoka eneo la ukambani. |
| Nyimbo zake ni za mtindo wa 'benga'. |
| Ken anaalbamu kadhaa na zote kwa lugha ya kikamba. |
| Chakushangaza ni kuwa nyimbo zake zinaumaarufu kwa watu wa maeneo yote nchini hata wasioelewa kikamba. |
| Majina yake kamili ni Ken Wambua Nguze. |
| Yeye anapenda kujitambulisha kama mfalme wa nyimbo za kikamba na kila mmoja aliyehudhuria tamasha zake unauhakika wa jambo hili. |
| Ken huongoza bendi maarufu inayojulikana kama 'Yatta Orchestra International Band.' |
| Tofauti na wanamuziki wengi waofanya muziki pekee, Ken ni mwanasiasa na mjasiriamali anayehusika hasa na nyumba za kukodisha. |
| Kama mjasiriamali, Ken amelipa shilingi milioni 3 kwa nyumba katika sehemu ya Doonholm, Nairobi; anamiliki maduka matatu ya nguo mjini , pia ni mshirika katika Kinga Motors Umoja, kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. |
| Yeye ni mmojawapo ya watu wanaomiliki kampuni ya Sunset Safaris - Pur jijini Mombasa. |
| Azimio la Ken wa Maria kuwania kiti cha ubunge lilikatika alipopokea vitisho vya kuuliwa kutoka kwa wanaodhaniwa kuwa wapinzani wake. |
| Hivyo basi, aliamua kumuunga mkono kiongozi wake katika siasa mheshimiwa Kalonzo Musyoka aliyekuwa mgombea mwenza Mheshimiwa Raila Odinga ambaye ni kiongozi wa chama cha muungano wa CORD. |
| Ken ambaye sasa anaumri wa miaka 36 ana mke na watoto wawili. |
| Licha ya muziki wake kupata soko kubwa mandarini, Ken hajawai onekana katika vyombo vya habari wala kujulikana kama mwana mziki aliyesifika sana lakini mambo haya hayamtishi moyo. |
| Katika mwaka wa 2001 Ken aliteuliwa kama mmoja wa waliokuwa wakigombea taji la East Africa Music Awards katika jamii ya nyimbo za mtindo wa kilingala. |
| Kulingana na yeye kuteuliwa kwake ni jambo la kutosha la kuonyesha kuwa muziki wake unafanya vizuri hata kama hajaweza kupata tuzo hilo. |
Comments
Hide