| Joseph Kamaru |
| Joseph Kamaru ni mwana muziki wa Benga kutoka sehemu ya kati ya Kenya. |
| Alizaliwa mwaka 1939 katika jamii ya wakikuyu kule Kangema kaunti ya Murang’a. |
| Awali, Kamaru alikuwa msaadizi wa nyumbani mjini Nairobi. |
| Alipata kazi hii mwaka wa 1957. |
| Baadaye katika mwaka 1965, Joseph Kamaru alianza kazi ya muziki na tangu wakati huo, ameuza karibu nusu milioni ya rekodi zake. |
| Wimbo wa Mwangi Gachau ulimpea motisha wa kufikiria kuwa anaweza kufanya vyema zaidi yake. |
| Mnamo wa mwaka wa 1967, wimbo wake wa `Celina ' ulivuma sana na kumfanya kupenya katika muziki. |
| Yeye ndiye mwanamuziki wa kwanza Kenya kuwa na maonyesho Carnivore. |
| Hivi ndivyo alivyofungulia wanawaziki wengine wa wakenya lango la kuonyesha Carnivore. |
| Kazi yake ilifikia kilele kati ya mwaka 1975 na 1985. |
| Nyimbo zake zilikuwa za kisiasa na uhusiano wake na rais wa wakati huo, rais Jomo Kenyatta ulikuwa imara na wa karibu. |
| Baada ya kifo cha Yosia Mwangi Kariuki, Kamaru alikashifu kifo hicho na hili lilihofisha uhusiano wake wa karibu na Kenyatta. |
| Ujasiri wake ulirejeshwa mwaka wa 1980 na rais wa pili wa Kenya, Bwana Moi. |
| Alikuwa miongoni mwa walioandamana na rais Moi nchini Japani. |
| Kamaru aliunga mkono serikali ya viama mbalimbali jambo ambalo lilimkasirisha rais. |
| Baadaye katika mwaka wa 1993, Kamaru aligeukia muziki wa injili na kuliacha kundi lake liitwalo ‘Kamaru supersounds.’ |
| Hili iliathiri umaarufu wake. |
| Hata hivyo, hakujutia uamuzi wake. |
| Yeye ni mwenyekiti wa Chama cha Kenya cha Viwanda vya senturi. |
| Pia, anamiliki huduma ya kanisa mjini Nairobi, ambako ana maduka ya rekodi mbili. |
Comments
Hide