| Kuja kuzaliwa | 
                                                                
                                                                            | Hiki kitabu  cha kuvutia kimeandikwa na Marjorie Oludhe Macgoye mzaliwa wa uingereza ambaye amekuwa mkazi wa nchi ya Kenya kwa muda mrefu. | 
                                                                
                                                                            | Wahusika wakuu katika hii hadithi ni Martin na mkewe Paulina ambao wamefunga ndoa hivi karibuni. | 
                                                                
                                                                            | Katika mwanzo wa hadithi, Paulina ambaye ana umri wa miaka 16 ni mjamzito. | 
                                                                
                                                                            | Anasafiri kutoka kijijini hadi mji mkuu wa Nairobi kujiunga na mumewe anayeishi na kufanya kazi Kariokor. | 
                                                                
                                                                            | Inatokea kwamba baada ya siku chache, Paulina anakuwa mgonjwa na kupelekwa katika hospitali ya pumwani. | 
                                                                
                                                                            | Kwa bahati mbaya ile mimba inatoka. | 
                                                                
                                                                            | Analazwa hospitalini lakini siku ya pili anaamua kutoka na kuelekea nyumbani bila kumngojea mumewe. | 
                                                                
                                                                            | Kwa bahati mbaya anapotea njia na kwasababu hafanikiwi kufika nyumbani, inamlazimu aishi nje kwa siku mbili. | 
                                                                
                                                                            | Hatimaye, Martin anampata lakini amekasirika kwavile Paulina hakumngojea. | 
                                                                
                                                                            | Usiku huo na kwa mara ya kwanza anamchapa bibiye. | 
                                                                
                                                                            | Hadithi hii inaendelea na Paulina anapata mimba zingine lakini zote zinatoka kabla ya wakati wa kujifungua. | 
                                                                
                                                                            | Ndoa yao inazidi kuwa ngumu, na kutofautiana pia kunaongezeka. | 
                                                                
                                                                            | Martin anaanza kutokuwa mwaminifu na kuanza uhusiano na wanawake wengine. | 
                                                                
                                                                            | Paulina naye anaamua  kumuacha na kuelekea Kisumu. | 
                                                                
                                                                            | Huko anafanikiwa kupata kazi ya uwalimu. | 
                                                                
                                                                            | Naye pia anabadilisha mienendo na kuanza kuhusishana na mwanaume mwingine. | 
                                                                
                                                                            | Chakushangaza ni kuwa wakati huu anafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume. | 
                                                                
                                                                            | Furaha yake inakatizwa wakati mtoto huyu anauliwa na polisi wanapofyatulia umati risasi katika mji wa Kisumu. | 
                                                                
                                                                            | Paulina anaamua kurudi Nairobi ambapo anaajiriwa kama mjakazi kwa tajiri mmoja ambaye yuko katika harakati za siasa. | 
                                                                
                                                                            | Martin anaanza kumtembelea Paulina na wakati kitabu hiki kinamalizika wameshakuwa mume na mke tena. | 
                                                                
                                                                            | Mara hii, Paulina anafanikiwa kumpa Martin mtoto. | 
                                                        
                     
Comments
Hide