| Kuja kuzaliwa |
| Hiki kitabu cha kuvutia kimeandikwa na Marjorie Oludhe Macgoye mzaliwa wa uingereza ambaye amekuwa mkazi wa nchi ya Kenya kwa muda mrefu. |
| Wahusika wakuu katika hii hadithi ni Martin na mkewe Paulina ambao wamefunga ndoa hivi karibuni. |
| Katika mwanzo wa hadithi, Paulina ambaye ana umri wa miaka 16 ni mjamzito. |
| Anasafiri kutoka kijijini hadi mji mkuu wa Nairobi kujiunga na mumewe anayeishi na kufanya kazi Kariokor. |
| Inatokea kwamba baada ya siku chache, Paulina anakuwa mgonjwa na kupelekwa katika hospitali ya pumwani. |
| Kwa bahati mbaya ile mimba inatoka. |
| Analazwa hospitalini lakini siku ya pili anaamua kutoka na kuelekea nyumbani bila kumngojea mumewe. |
| Kwa bahati mbaya anapotea njia na kwasababu hafanikiwi kufika nyumbani, inamlazimu aishi nje kwa siku mbili. |
| Hatimaye, Martin anampata lakini amekasirika kwavile Paulina hakumngojea. |
| Usiku huo na kwa mara ya kwanza anamchapa bibiye. |
| Hadithi hii inaendelea na Paulina anapata mimba zingine lakini zote zinatoka kabla ya wakati wa kujifungua. |
| Ndoa yao inazidi kuwa ngumu, na kutofautiana pia kunaongezeka. |
| Martin anaanza kutokuwa mwaminifu na kuanza uhusiano na wanawake wengine. |
| Paulina naye anaamua kumuacha na kuelekea Kisumu. |
| Huko anafanikiwa kupata kazi ya uwalimu. |
| Naye pia anabadilisha mienendo na kuanza kuhusishana na mwanaume mwingine. |
| Chakushangaza ni kuwa wakati huu anafanikiwa kujifungua mtoto wa kiume. |
| Furaha yake inakatizwa wakati mtoto huyu anauliwa na polisi wanapofyatulia umati risasi katika mji wa Kisumu. |
| Paulina anaamua kurudi Nairobi ambapo anaajiriwa kama mjakazi kwa tajiri mmoja ambaye yuko katika harakati za siasa. |
| Martin anaanza kumtembelea Paulina na wakati kitabu hiki kinamalizika wameshakuwa mume na mke tena. |
| Mara hii, Paulina anafanikiwa kumpa Martin mtoto. |
Comments
Hide