| SIKU NJEMA | 
                                                                
                                                                            | Hii ni hadithi iliyoandikwa na mwandishi anayejulika sana kwa uadishi wa riwaya wa lugha ya kiswahili. | 
                                                                
                                                                            | Anajulikana kama  Ken Walibora. | 
                                                                
                                                                            | Mhusika mkuu  katika riwaya hii ni Msanifu Kombo ambaye baadaye alipata jina Kongowea Mswahili baada ya kushinda tuzo katika mashindano ya utunzi. | 
                                                                
                                                                            | Mazingira ya hadithi ni Tanga nchi Tanzania. | 
                                                                
                                                                            | Kombo anakabiliwa na matatizo  mengi maana alikuwa na mzazi mmoja tu, mamake Zainabu Makame. | 
                                                                
                                                                            | Bi.Makame alikuwa mwimbaji wa muziki wa kitaarab, maarufu nchini Tanzania na katika mkoa wa pwani wa Kenya. | 
                                                                
                                                                            | Kutokuwa na baba mzazi kwa Kombo kulivutia ubaguzi mwingi hasa kutoka kwa  wanafunzi wenzake shuleni. | 
                                                                
                                                                            | Kitamaduni, kutokuwa na baba mzazi unayemjua ilikuwa  jambo lisilokubalika. | 
                                                                
                                                                            | Mambo yalizidi kuwa magumu kwa Kombo baada ya mamake kufa. | 
                                                                
                                                                            | Alilelewa na shangazi yake na mama wa kambo ambao walimdhulumu sana. | 
                                                                
                                                                            | Ubanguzi shuleni na dhuluma nyumbani ulifanya maisha yake kuwa magumu. | 
                                                                
                                                                            | Licha ya hayo yote yeye ni mwandishi mwenye kipaji. | 
                                                                
                                                                            | Ni jambo hili alilotumia kuwashinda wenzake na kumfanya mwanafunzi mwenye umaarufu shuleni. | 
                                                                
                                                                            | Baadaye, aliamua kutorokea nchini Kenya kumtafuta babake mzazi ambaye alikuwa amemwona kwa picha tu. | 
                                                                
                                                                            | Juhudi zake hazikuwa za bure kwa kuwa mwishowe aliweza kumpata. | 
                                                                
                                                                            | Babake alikuwa mshairi maarufu aliyejulikana kama Juma Mkosi. | 
                                                                
                                                                            | Hata hivyo watu wengi walimjua kwa jina lake la ushairi Amju Aiskom ambalo  ni endelezo la jina lake likiwa limeanziwa kutoka nyuma. | 
                                                                
                                                                            | Wakati hadithi hii inafikia mwisho, siku njema inamjia Kongowea  kwa ajili ya kumpata babake mzazi na kwa wakati huu ameshaoa Vumilia Binti Abdulla. | 
                                                                
                                                                            | Anaendelea na hamu ya kuandika kwani anaonekana kana kwamba amekuwa akiandika kitabu hiki usiki mzima. | 
                                                                
                                                                            | Kitabu hiki kinadhaniwa kinamhusu bibiye anayetokezea kwa nyuma na kumkumbatia, hapo ndipo linamdua kuwa jua limeshachomoza. | 
                                                        
                     
Comments
Hide