Dialogue

Vocabulary

Learn New Words FAST with this Lesson’s Vocab Review List

Get this lesson’s key vocab, their translations and pronunciations. Sign up for your Free Lifetime Account Now and get 7 Days of Premium Access including this feature.

Or sign up using Facebook
Already a Member?

Lesson Transcript

Hamjamboni, mimi ni Medina.
Sikukuu ya kimataifa ya maonyesho ya biashara Kenya hufanyika nyakati tofauti kila mwaka. Siku hii ni nafasi njema inayotumiwa na mashirika ya humu nchini na yale ya kimataifa kujiinua kibiashara. Maonyesho haya hufanyika katika Jumba Kuu la Mikutano la Kimataifa la Kenyatta.
Kupitia video hii, utaelimika kuhusu kinachotendeka katika maonyesho haya.
Je, unajua ni bidhaa zipi hupatikana kwa wingi sana katika maonyesho haya?
Tutawaonyesha jibu la swali hili mwishoni mwa video hii.
Katika maonyesho haya bidhaa za sekta nyingi hukusanyika hapa. Soko la Afrika mashariki ikiwamo na vyombo tofauti na mashine pia hukusanywa. Zaidi ya wanabiashara mia moja na hamsini hutandaza vitu vyao mahala pakubwa kupita mita elfu tatu.
Baada ya kila sehemu ya maonyesho, karamu huandaliwa ili kuwasaidia waonyeshaji kuongea na kujuana na wenzao ambao hukuja kutoka nchi za mbali kuona bidhaa hizi. Ushirikiano wa kudumu wakibiashara hutengenezwa. Waliohudhuria hubadilishana anwani, namba za simu na hupata kugundua jinsi wanavyoweza kufanya biashara pamoja. Wasio kuwa na ujuzi hupata kuwa wajuzi kupitia shughuli hii.
Nia moja ya Sikukuu ya kimataifa ya maonyesho ya biashara nchini Kenya ni kuwaleta pamoja wanunuzi na wauzaji wa bidhaa na huduma tofauti. Maonyesho haya huvutia waundaji wakuu katika sekta zao pamoja na wanunuzi wa maana sana.
Kutoka idara ya hoteli na mikahawa, washika ndao wote hupata fursa ya kuonyesha miundo yao ya kipekee na ubunifu mpya. Wageni wanaohudhuria ni mameneja wakuu, wanunuzi, waakilishi wa serikali na washauri.
Na sasa nitawapa jibu la swali la hapo awali.
Je, unajua ni bidhaa zipi hupatikana kwa wingi sana katika maonyesho haya?
Baadhi ya bidhaa ambazo hupatikana kwa wingi ni kama vile bidhaa za stima, za ujenzi, za vitambaa za nguo, za teknolojia, za afya na hata maelezo ya kupika chakula tofauti.
Funzo hili lilikuwaje? Je, ulijiifunza jambo lolote la kusisimua?
Je, nchini mwako kuna maonyesho ya kibiashara kama haya?
Tuwachie maoni yako katika SwahiliPod101.com kisha tuonane katika somo lifuatalo!

Comments

Hide