| Ken wa Maria | 
                                                                
                                                                            | Ken wa Maria anafanya muziki wake  katika lugha ya kikamba. | 
                                                                
                                                                            | kwa sasa yeye ndiye msanii mmaarufu kutoka eneo la ukambani. | 
                                                                
                                                                            | Nyimbo zake ni za mtindo wa 'benga'. | 
                                                                
                                                                            | Ken anaalbamu kadhaa na zote kwa lugha ya kikamba. | 
                                                                
                                                                            | Chakushangaza ni kuwa nyimbo zake zinaumaarufu kwa watu wa maeneo yote nchini hata wasioelewa kikamba. | 
                                                                
                                                                            | Majina yake kamili ni Ken Wambua Nguze. | 
                                                                
                                                                            | Yeye anapenda kujitambulisha kama mfalme wa nyimbo za kikamba na kila mmoja aliyehudhuria tamasha zake unauhakika wa jambo hili. | 
                                                                
                                                                            | Ken huongoza bendi maarufu inayojulikana kama 'Yatta Orchestra International Band.' | 
                                                                
                                                                            | Tofauti na wanamuziki wengi waofanya muziki pekee, Ken ni mwanasiasa na mjasiriamali anayehusika hasa na nyumba za kukodisha. | 
                                                                
                                                                            | Kama mjasiriamali, Ken amelipa shilingi milioni 3 kwa nyumba katika sehemu ya Doonholm, Nairobi;  anamiliki maduka matatu ya nguo mjini , pia ni mshirika katika Kinga Motors Umoja, kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. | 
                                                                
                                                                            | Yeye ni mmojawapo ya watu wanaomiliki kampuni ya Sunset Safaris - Pur jijini Mombasa. | 
                                                                
                                                                            | Azimio la Ken wa Maria kuwania kiti cha ubunge lilikatika alipopokea vitisho vya kuuliwa kutoka kwa wanaodhaniwa kuwa wapinzani wake. | 
                                                                
                                                                            | Hivyo basi, aliamua kumuunga mkono kiongozi wake katika siasa mheshimiwa Kalonzo Musyoka aliyekuwa mgombea mwenza Mheshimiwa Raila Odinga ambaye ni kiongozi wa chama cha muungano wa CORD. | 
                                                                
                                                                            | Ken ambaye sasa anaumri wa miaka 36 ana mke na watoto wawili. | 
                                                                
                                                                            | Licha  ya muziki wake kupata soko kubwa mandarini, Ken hajawai onekana katika vyombo vya habari wala kujulikana kama mwana mziki aliyesifika sana lakini mambo haya hayamtishi moyo. | 
                                                                
                                                                            | Katika mwaka  wa 2001 Ken aliteuliwa kama mmoja wa waliokuwa wakigombea taji la East Africa Music Awards katika  jamii  ya nyimbo za mtindo wa kilingala. | 
                                                                
                                                                            | Kulingana na yeye kuteuliwa kwake ni jambo la kutosha la kuonyesha kuwa muziki wake unafanya vizuri hata kama hajaweza kupata tuzo hilo. | 
                                                        
                     
Comments
Hide