| Joseph Kamaru | 
                                                                
                                                                            | Joseph Kamaru ni mwana muziki wa  Benga kutoka sehemu ya kati ya Kenya. | 
                                                                
                                                                            | Alizaliwa mwaka 1939 katika jamii ya wakikuyu kule Kangema kaunti ya Murang’a. | 
                                                                
                                                                            | Awali, Kamaru alikuwa msaadizi wa  nyumbani mjini Nairobi. | 
                                                                
                                                                            | Alipata kazi hii mwaka wa 1957. | 
                                                                
                                                                            | Baadaye katika mwaka 1965, Joseph Kamaru alianza kazi ya muziki na tangu wakati huo, ameuza  karibu nusu milioni ya rekodi zake. | 
                                                                
                                                                            | Wimbo wa Mwangi Gachau ulimpea motisha wa kufikiria kuwa anaweza kufanya vyema zaidi yake. | 
                                                                
                                                                            | Mnamo wa mwaka wa 1967, wimbo wake wa `Celina ' ulivuma sana  na kumfanya kupenya katika muziki. | 
                                                                
                                                                            | Yeye ndiye mwanamuziki wa kwanza Kenya kuwa na maonyesho Carnivore. | 
                                                                
                                                                            | Hivi ndivyo alivyofungulia wanawaziki wengine wa wakenya lango la kuonyesha Carnivore. | 
                                                                
                                                                            | Kazi yake ilifikia kilele kati ya mwaka 1975 na 1985. | 
                                                                
                                                                            | Nyimbo zake zilikuwa za kisiasa na uhusiano wake na rais wa wakati huo, rais Jomo Kenyatta ulikuwa imara na wa karibu. | 
                                                                
                                                                            | Baada ya kifo cha Yosia Mwangi Kariuki, Kamaru alikashifu kifo hicho na hili lilihofisha uhusiano wake wa karibu na Kenyatta. | 
                                                                
                                                                            | Ujasiri wake ulirejeshwa mwaka wa 1980 na rais wa pili wa Kenya, Bwana Moi. | 
                                                                
                                                                            | Alikuwa miongoni mwa walioandamana na rais Moi nchini Japani. | 
                                                                
                                                                            | Kamaru aliunga mkono serikali  ya viama mbalimbali jambo ambalo lilimkasirisha rais. | 
                                                                
                                                                            | Baadaye katika mwaka wa 1993, Kamaru aligeukia  muziki wa injili na kuliacha kundi lake liitwalo ‘Kamaru supersounds.’ | 
                                                                
                                                                            | Hili iliathiri  umaarufu wake. | 
                                                                
                                                                            | Hata hivyo, hakujutia uamuzi wake. | 
                                                                
                                                                            | Yeye ni mwenyekiti wa Chama cha Kenya cha Viwanda vya senturi. | 
                                                                
                                                                            | Pia, anamiliki huduma ya kanisa mjini Nairobi, ambako ana maduka ya rekodi mbili. | 
                                                        
                     
Comments
Hide