| MTO NA CHANZO | 
                                                                
                                                                            | Hiki ni kitabu cha kuwezesha na wengi wanakiona kama wito wa uamsho hasa kwa wanawake. | 
                                                                
                                                                            | Hadithi hii inagusia vizazi vitatu vya kitamaduni na ya kisasa ya wanawake wa jamii ya wajaluo. | 
                                                                
                                                                            | Wahusika wakuu ni Akoko aliyezaliwa katika jamii ya utamaduni ya waluo, na mjukuu wake Awiti ambaye ameangazika pamoja na watoto wake wanaoishi katika karne ya ishirini na mmoja. | 
                                                                
                                                                            | Hadithi hii ya  kuvutia huanza na hadithi ya mapenzi ambapo Akoko, binti wa  pekee wa chifu mkuu  amefikia umri wa kuolewa. | 
                                                                
                                                                            | Kuna waposa wengi wanaotakakumchumbia. | 
                                                                
                                                                            | Mmoja wao amempenda zaidi hadi amekubali kulipa mahari ya ngo'mbe thelathini, kiwango cha juu sana wakati huo ambapo watu wachache wangemudu. | 
                                                                
                                                                            | Aliolewa na ndoa yao ilikuwa yenye raha hasa baada ya  kupata watoto  kama baraka ya Were aliyekua mungu wa jua. | 
                                                                
                                                                            | Hata hivyo, furaha hii haikuendelea kwa muda mrefu. | 
                                                                
                                                                            | Mumewe alifariki na kumwacha pamoja na wanawe. | 
                                                                
                                                                            | Matatizo yake yalianza wakati familia ya mumewe iliamua kumnyanganya mali aliyoachiwa. | 
                                                                
                                                                            | Akoko alichukua hatua na kwenda kwa serikali ambayo kwa wakati huo ilikuwa ya wa wazungu. | 
                                                                
                                                                            | Aliomba msaada, jambo ambalo halikuwa limefanywa na mtu yeyote. | 
                                                                
                                                                            | Juhudi zake hazikuwa za bure  kwani alisaidiwa baada ya uchunguzi na mali yake kurejeshwa. | 
                                                                
                                                                            | Bintiye, ambaye kwa sasa pia ni mjane alianza kuteswa na familia ya mumewe na akaamua kuenda kutafuta msaada kutoka kwa mungu anayewasaidia wajane na mayatima. | 
                                                                
                                                                            | Alienda hadi kwa kanisa ya misheni ya katoliki na kujiunga na imani yao. | 
                                                                
                                                                            | Mamake na dadake Awiti pia walijiunga naye. | 
                                                                
                                                                            | Awiti ni mwerevu na yuko miongoni mwa wasichana wawili wanaodhaminiwa kupata masomo katika koleji ya uwalimu. | 
                                                                
                                                                            | Baadaye anaoleka na kupata watoto saba ambao wanapata mafunzo ya utaalamu kama vile uhudumu wa hewa na utoaji damu. | 
                                                        
                     
Comments
Hide